Baada ya subira ya miaka tisa hatimaye klabu ya Hull City, ilirejea kwenye ligi kuu Uingereza Jumamosi jioni ilipowashinda Middlesbrough, bao moja kwa bila katika uwanja wa Wembley.
McBurnie alitumia makosa ya kipa wa Boro, Sol Brynn na kufunga bao la dakika ya 95,lililpowapa City ushindi.
Hull City ni timu ya sita kushinda mechi hiyo ya mchujo wa kupandishwa daraja katika Ligi Kuu Uingereza tangu mwaka 2010.
Hull City wanajiunga na Coventry City na Ipswich Town, katika Ligi Kuu Uingereza msimu wa mwaka 2026/2027.