Shirikisho la soka nchini Morocco (FRMF) limezindua kampuni ya Google Gemini, kama mshirika wa timu ya taifa ya Atlas Lions kwa fainali za Kombe la Dunia .
Ushirikiano huo uanjiri kama sehemu ya maandilizi ya Morocco, kwa fainali za Kombe la Dunia mwezi Juni na Julai, mwaka huu.
Ushirikiano huo wa kimkakati unalenga kuiwezesha Atlas Lions, kutumia Teknolojia ya AI ya Google Gemini, kurahisha utangamano wake na mashabiki kupitia mitandao ya kijamii na kukuza vipaji ndani na nje ya Morocco.
Google Gemini na FRMF, watashirikiana kuanzisha mitandao kadhaa ya kutangamana baina ya wachezaji na mashabiki kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya AI .
Kupitia ushirikiano huo mashabiki watapata fursa ya kusoma na kupata ufafanuzi wa sheria za mchezo ,kupata uchambuzi na ubashiri matokeo ya mechi.