Rais William Ruto amesema serikali inajenga nyumba 273,000, za gharama nafuu katika maeneo mbalimbali nchini huku nyingine 9,000, zikiwa zimekamilishwa na kukabidhiwa wamiliki.
Akiongoza sherehe za 61, za siku kuu ya Wafanyakazi siku ya Ijumaa,katika kaunti ya Vihiga, Ruto, ameongeza kuwa miradi sita ya nyumba za gharama nafuu inaendelea.
Mradi huo unatarajiwa kutoa vyumba 3,720, kwa gharama ya shilingi bilioni 7.5, punde utakapokamilika.
Ruto ameongeza kuwa mradi wa ujenzi wa vyumba vya wanafunzi kuishi unaendelea na utamudu jumla ya vitanda 4,540, kwa gharama ya shilingi bilioni 1.9, utakapokamilika.
Kiongozi wa nchini alesema pia serikali inajenga masoko mengine 10, huku mengine sita yakitarajiwa kujengwa.
Masoko hayo yatakuwa na vibanda 3,470 kwa wafanyabiashara .
Alisema kuwa serikali imeekeza jumla ya shilingi bilioni 15, kwa ujumla katika kaunti hiyo ya Vihiga.