Barabara ya Rironi-Mau Summit, kuanza kutumika Aprili mwaka ujao

Dismas Otuke
1 Min Read

Barabara ya Rironi-Mau Summit, itaanza kutumika na umma rasmi mwezi Aprili mwaka ujao.

Haya yametangazwa na Rais William Ruto siku ya Ijuamaa,alipoongoza sherehe za 61, za siku kuu ya Wafanyakazi katika kaunti ya Vihiga.

Alifichua kuwa tayari ujenzi unaendelea huku mkandarasi akifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha inakamilika kwa wakati ufaao.

Rais ameongeza kuwa watatoa kandarasi mpya ifikiapo mwishoni mwa mwaka huu  kwa upanuzi wa barabara hiyo kutoka Mau Summit hadi Malaba.

Ruto alisema kukamilishwa kwa barabara hiyo kutapunguza msongamano wa magari, ambao umekuwa ukishuhudiwa kwa kawaida.

Aidha,alisema kuwa kukamilishwa kwa barabara hiyo kutabuni nafasi za ajira zipatazo 10,000.

Alitaja kuwa kukamilishwa kwa barabaraba hiyo na pia reli ya SGR, kutafungua fursa nyingi za kibiashara na  kukuza uchumi wa Kenya.

Ruto amekariri kujitolea kwa serikali yake kukamilisha miundombinu muhimu humu nchini kwa manufaa ya Wakenya.

Share This Article