Wafanyakazi wapata nyongeza ya asilimia 12 ya mshahara

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto ametangaza nyongeza ya mshahara wa wafanyakazi kwa asilimia 12, katika sherehe za 61, za siku kuu ya Leba Dei.

Sherehe hizo  sherehe zimeandaliwa Ijumaa katika  shule ya Chavakali Boys, kaunti ya Vihiga.

Pia Rais, ametangaza nyongeza ya silimia 15, kwa mshahara wa wafanyakazi wa sekta ya kilimo.

Aidha,Ruto ametoa hakikisho la kuboresha  maslahi  ya wafanyakazi .

Sherehe za Leba Dei, zimeandaliwa leo kwa mara ya kwanza nje ya kaunti ya Nairobi, na zilihudhuriwa na viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini pamoja na viongozi wakuu serikalini.

 

Share This Article