Serikali ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania, imeapa kulipiza kisasi na kupiga marufuku bidhaa za kilimo na mazao kutoka Afrika Kusini na Malawi, kulipiza kisasi baada ya mataifa hayo kuiwekea Tanzania vikwazo.
Tanzania imesema itaweka vikwazo hivyo kuanzia tarehe Aprili 23.2025, kulingana na taarifa ya Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.
Serikali ya Tanzania imekuwa iking’ang’ana kuuza bidhaa zake zikiwemo ndizi katika soko la Kusini mwa Afrika.
Aidha Waziri amewaarifu wakulima kusitisha kupakia bidhaa zao zinazopaniwa kuuzwa katika masoko hayo ya Kusini mwa Afrika hadi hali itakapokuwa shwari.