Kenya inajitahidi kuondolewa kwa marufuku ya uuzaji Majani Chai chini

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe ashiriki mazungumzo na wafanfabiashara wa Iran kuhusu Majani Chai kutoka Kenya.

Serikali inajizatiti kufanikisha juhudi zake za kutaka marufuku dhdi ya uuzaji Majani Chai nchini Iran yaondolewe, kwa lengo la kuwezesha bidhaa hiyo ya Kenya kufunguliwa milango tena katika soko hilo la kumezewa mate.

Akizungumza leo Alhamisi alipokutana na wafanyabiashara kutoka Iran, waziri wa Kilimo na Ustawi wa Mifugo Mutahi Kagwe, alidokeza kuwa Kenya imejitolea kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na kuhakikisha Majani Chai ya ubora wa juu yanafika katika masoko ya kimataifa.

“Kufunguliwa tena soko la Irani, kutawanufaisha wakulima wa Majani Chai na mfumo mzima wa zao hilo,” alisema Kagwe.

Wakati wa mkutano huo, viongozi hao walijadili kuhusu kupanuliwa kwa fursa za biashara sio tu nchini Iran, lakini pia  katika kanda nzima ya Mashariki ya Kati na Katikati ya bara Asia.

Katika mkutano huo, waziri Kagwe alikuwa ameandamana na balozi wa Kenya katika Muungano wa Milki za Kiarabu Kenneth Milimo, mwenyekiti wa shirika la maendeleo ya Majani Chai nchini (KTDA) Chege Kirundi na Afisa Mkuu Mtendaji wa shirika hilo Wilson Muthaura.

Kulingana na Bodi ya Majani Chai nchini (TBK), mnamo mwaka 2024, pato jumla kutoka kwa Majani Chai lilikuwa shilingi bilioni 215.21 Billion, ambapo shilingi bilioni 181.69 yalitokana na mauzo katika masoko ya nje.

Website |  + posts
Share This Article