Kocha wa Ujermani, Julian Nagelsmann ang’atuka

Jurgen Klopp aliyekuwa kocha wa Liverpool anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha mpya wa Ujerumani baada ya kuafikiana na shirikisho la soka nchini Ujerumani kuhusu vipengee vingi vya mkataba wake.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kocha wa Ujerumani Julian Nagelsmann,amejiuzulu siku nne baada ya timu yake kutimuliwa kwenye raundi ya 16, ya Kombe la Dunia na Paraguay, katika matuta ya penati.

Nagelsmann aliye na umri wa miaka 38, alitwaa ukufunzi wa Ujerumani kutoka kwa Hansi Flick, Septemba mwaka 2023, na kuingoza hadi kwota fainali ya Kombe la Euro mwaka 2024,wakiwa nyumbani na kufikia nusu fainali ya UEFA Nations League, mwaka 2025.

Jurgen Klopp aliyekuwa kocha wa Liverpool anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha mpya wa Ujerumani, baada ya kuafikiana na shirikisho la soka nchini Ujerumani kuhusu vipengee vingi vya mkataba wake.

Share This Article