Morocco yaendelea kushamiri katika soka duniani baada ya kumtwaa mchezaji Ayyoub Bouaddi

Kando na ujuzi na ufundi utakaoletwa na kiungo huyo wa klabu ya Lille katika timu ya Atlas Lions ,hatua iliyochukuliwa na Bouaddi, inaashiria maendeleo na ufanisi mkubwa katika soka ya Morocco sio tu barani Afrika bali ulimwenguni kote.

Dismas Otuke
1 Min Read

Tangazo la shirikisho la soka nchini Morocco (FRMF) kuhusu kubadilisha kwa uraia wa mchezaji Ayyoub Bouaddi, na kukubali kuichezea Atlas Lions ni dhihirisho la hatua kubwa iliyopigwa na taifa hilo la kaskazini mwa Afrika katika kandanda.

Kando na ujuzi na ufundi utakaoletwa na kiungo huyo wa klabu ya Lille katika timu ya Atlas Lions ,hatua iliyochukuliwa na Bouaddi, inaashiria maendeleo na ufanisi mkubwa katika soka ya Morocco sio tu barani Afrika bali ulimwenguni kote.

Morocco imejitangaza kama mojawapo wa mataifa yenye ushindani katika soka na yanayofanya vyema na yenye uwezo wa kuwavutia wachezaji tajika walio na uraia mara mbili ili kurejea nyumbani.

Ufanusu  huo umetokana na juhudi na mfumo wa soka ya Morocco unaoongozwa na Mfalme Mohammed wa sita.

Chini ya uongozi wa Mfalme Morocco imekuwa mfano bora kwa mataifa mengi ya Afrika katika mikakati iliyowekwa ya ukuzaji soka .

Mfumo wa Morocco katika soka unatoa fursa za ukuzaji vipaji na mifumo inayoambatana na viwango vya kimataifa ambayo vimekuwa vivutio muhimu.

Bouddi alizaliwa nchini Ufaransa  na amezichezea timu za taifa za Ufaransa chini ya umri wa miaka 16,miaka 17,miaka 18,miaka 19 na chini ya miaka 20.

Share This Article