Mabingwa watetezi wa taji ya Ligi ya Mabingwa ulaya, Real Madrid watachuana na mabingwa wa Uingereza Manchester City katika mchujo wa kuwania tiketi ya kucheza raundi ya 16 bora.
Vijana wa Pep Guardiola wataandaa mkumbo wa kwanza kati ya Februari 12 na 13 huku marudio yakiandaliwa baina ya Februari 17 na 18.
Kwa mujibu wa droo iliyoandaliwa Ijumaa, Atletico Madrid ya Uhispania watakumbana na mabingwa wa Ujerumani Bayer Leverkusen.
Katika mechi nyingine mabingwa wa Ufaransa PSG watachuana na Brest pia ya Ufaransa, Benfica kutoka Ureno wawatumbuize Monaco ya Ufaransa wakati Juventus wakitoana jasho na PSV Eindhoven.
Mabingwa mara saba AC Milan kutoka Italia watapambana na Feyenoord ya Uholanzi, Bayern Munich kutoka Ujerumani walioshinda kombe hilo mara 6, wakipangwa dhidi ya mabingwa wa Scotland, Celtic.
Sporting Lisbon ya Ureno itamenyana na Borussia Dortmund ya Ujerumani, huku Club Brugge kutoka Ubelgiji wakiwa na miadi dhidi ya Atalanta Bergamo ya Italia.
Droo ya raundi 16 itaandaliwa terehe 21 mwezi ujao.
Duru ya kwanza ya raundi ya 16 bora itaandaliwa kati ya Machi 4 na 5 huku marudio yaliandaliwa wiki moja baadaye.
Robo fainali itasakatwa kati ya tarehe 8 na 9 Aprili na marudiano Aprili 15 na 16.
Duru ya kwanza ya semi fainali imepangiwa tarehe 29 na 30 huku marudio ikiwa wiki moja baadaye.
Fainali itaandaliwa Mei 31 katika uwanja wa Munich nchini Ujerumani.