Kaunti ya Baringo imetangazwa kuwa mwenyeji wa makala ya 36, ya mashindano ya magari ya Rhino Charge mwaka huu.
Mashindano hayo ambayo hushirikisha magari ya four wheel yanayoshindana mbugani, yanalenga kuchangisha pesa za kuhifadhi mbuga za wanyamapori na vyanzo vya maji
Tangazo hilo limetolewa leo na karani wa mkondo wa mashindano hayo Don White,katika hafla ya uzinduzi iliyoandaliwa katika shule ya Braeburn kaunti ya Nairobi , na kuhudhuriwa na madereva,wafadhili,maafisa waandalizi,wasimamizi wa kambi na makarani wa mkondo.
Mashindano hayo yanayoandaliwa na shirika la Rhino Ark Charitable Trust, huchangisha mamilioni ya pesa kila mwaka ambazo huelekezwa kwa kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji ikiwemo Aberdare Range, Mt. Kenya,msitu wa Mau na ule wa Kakamega.