Kenya,Uganda na Tanzania kuafikiana kuhusu viwanja vya mechi za CHAN

Upande wao, Mawaziri wa michezo wa Uganda, Peter Ogwang, na mwenzake wa Tanzania, Hamisi Mwinjuma, walikariri kujitolea kwa mataifa yao kuandaa fainali za kufana.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya, Uganda na Tanzania zinatarajiwa kuafikiana kuhusu viwanja vitakavyotumika kuandaa mechi za fainali za nane za Kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN mwezi Agosti mwaka huu.

Haya yametangazwa leo na Waziri wa Michezo Salim Mvurya ,baada ya kufanya kikao kupitia mtandao na Katibu Mkuu wa shirikisho la soka barani Afrika CAF, Veron Mosengo Omba, pamoja na Mawaziri wa Michezo wa Uganda na Tanzania.

Kulingana na Mvurya, mataifa hayo matatu yataafikiana na kutangaza viwanja vitakavyotumika kwa sherehe za ufunguzi na kufunga michuano hiyo, mechi ya ufunguzi, fainali na ile ya nafasi ya tatu na nne.

Aidha, waziri wa alikariri mikakati iliyowekwa na serikali ya Kenya kudhihirisha kuwa tayari kuandaa CHAN, ikiwemo viwanja vinavyoafiki viwango vya kimataifa na kulipa ada ya maandalizi inavyohitajika.

Upande wao, Mawaziri wa michezo wa Uganda, Peter Ogwang, na mwenzake wa Tanzania, Hamisi Mwinjuma, walikariri kujitolea kwa mataifa yao kuandaa fainali za kufana.

Kipute cha CHAN kitaandaliwa kati ya Agosti 2 na 30 mwaka huu.

Website |  + posts
Share This Article