Serikali yaongeza maradufu ada ya kutumia huduma ya eCitizen

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali imeongeza maradufu ada ya kufanyia malipo kupitia kwa huduma ya eCitizen katika hatua inayolenga kuongeza kipato chake.

Kulipia huduma kupitia eCitizen kwa shilingi 100,000, na zaidi kutagharimu ada ya shilingi 100.

Malipo ya kati ya shiling10,000 na  shilingingi 99,000, yatakuwa na gharama ya shilingi 70.

Kulipia huduma za kati ya shilingi 500 na shilingi 9,999, kutakuwa na gharama ya shilingi 50, wakati gharama ya kulipia huduma za shilingi 100 hadi chini ya shilingi 499, zikilipishwa ada ya shilingi 5.

Hata hivyo, malipo yaliyo chini ya shilingi 100 hayatozwi gharama yoyote.

Awali huduma zote za kufanyia malipo ya kiwango chochote kupitia mtandao wa eCitizen, zimekuwa zikilipishwa kiwango cha wastani cha shilingi 50.

TAGGED:
Share This Article