UDA yabuni kamati ya kutatua mizozo ya uteuzi wa Ol Kalou

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama tawala nchini Kenya cha United Democratic Alliance (UDA), kimeunda kamati ya kusuluhisha mizozo na malalamishi yatakayotakana na uteuzi wa eneo bunge la Ol Kalou, kesho Ijumaa.

Katika notisi iliyotolewa Jumatano Mei 6, UDA ilisema malalamishi yote yatakayotokana na uteuzi huo ni sharti yawasilishwe ndani ya saa 24 baada kutangazwa kwa matokeo.

Bodi ya kitaifa ya uchaguzi aidha,imesema kuwa uteuzi huo utafanyika katika vituo vyote vya eneo bunge hilo.

Share This Article