Morocco yafungua kambi mpya ya Kombe la Dunia katika Jimbo la New Jersey nchini Marekani

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Morocco, imefungua kambi ya fainali za Kombe la Dunia, katika Jimbo la New Jersey nchini Marekani.

Gavana wa Jimbo hilo Mikie Sherrill aliandamana na Balozi wa Morocco nchini Marekani Youssef Amrani,katika hafla ya kufungua Kambi hiyo.

Kambi hiyo itakuwa makao ya Morocco, wakati wote wa fainali za Kombe la Dunia, kati ya mwezi ujao na Julai mwaka huu .

Morocco walitumia kambi hiyo katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 1994, kabla ya kufanyiwa ukarabati mwaka Jana ikijumuisha viwanja viwili vya nyasi.

Kambi hiyo inatarajiwa kutoka mazingira bora kwa Morocco maarufu kama Atlas Lions, wakijiandaa kwa mechi ya ufunguzi dhidi ya Brazil tarehe 13 mwezi ujao katika uwanja wa MetLife.

Gavana Sherrill, alisema kambi hiyo ni muhimu hususan kwa jimbo hilo lenye takriban raia 10,000 wa Morocco wanaoishi New Jersey.

Balozi wa Morocco aliishukuru Marekani,kwa kuwatengea kambi hiyo iliyo na vifaa vya kisasa kufanyia mazoezi.

Share This Article