Dessert Foxes ya Algeria imekuwa timu ya tisa ya Afrika, kufuzu kwa raundi ya 32 bora ya Kombe la Dunia, baada ya kulazimisha sare ya mabao 3 dhidi ya Austria, katika mchuano wa kundi J mapema Jumapili.
Riyad Mahrez alicheka na nyavu mara mbili naye Rafik Belghali akaongeza moja kwa Algeria.
Mzee wa kazi Marko Arnautovic,Marcel Sabitzer na Sasa Kalajdzic waliwajibika katika upachikaji magoli ya Austria.
Ushindi huo ulihakikisha mbweha hao wa jangwani wanaingia awamu ya 32, kwa kuwa miongoni mwa timu bora za nafasi ya tatu wakizoa alama 4.
Algeria wameratibiwa kumenyana na Uswizi katika hatua ya 32 bora Julai 3,wakifuzu kwa mwondoano kwa mara ya pili tangu mwaka 2014 nchini Brazil.
Algeria wanajiunga na Ghana,Morocco,Misri,Ivory Coast,Senegal,Afrika Kusini DR Congo na Cape Verde, ambazo zimetinga raundi hiyo ya 32.