Wekundu wa Canada kufungua mchujo wa Kombe la Dunia dhidi ya Bafana Bafana ya Afrika Kusini

Michuano 16 ya raundi ya 32 bora inayoshirikisha mataifa tisa ya Afrika itakamilika Julai 4.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kufuatia kukamilika kwa mechi 72 za hatua ya makundi, kipute cha Kombe la Dunia kitaingia mchujo wa raundi ya 32 leo nchini Canada, wakikabiliana na Bafana Bafana kutoka Afrika Kusini.

Mchuano huo utang’oa nanga saa nne usiku katika uwanja wa Sofi mjini California, Marekani.

Wekundu wa Canada wamelazimika kucheza ugenini, baada ya kumaliza katika nafasi ya pili kundini B,nyuma ya Uswizi.

Canada wamepigwa jeki na kurejea kwa nahodha Alphonso Davies aliyejeruhiwa wakati wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSG.

Afrika Kusini iliyoponea chupuchupu kutimuliwa baada ya kuwashinda Korea Kusini katika mechi ya mwisho ya kundi A, itakosa huduma za kiungo Themba Swane aliyepigwa kadi nyekundu katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Mexico.

Michuano 16 ya raundi ya 32 bora inayoshirikisha mataifa tisa ya Afrika itakamilika Julai 4.

Share This Article