Wakazi wa Laikipia walijitisa barabarani siku ya Jumatatu kufanya maandamano ya kupinga hatua ya kuwekwa kwa Karantini, ya wagonjwa wa Ebola, kwenye kambi ya wanajeshi wa Marekani iliyo eneo hilo.
Wananchi walioandamana walihoji usalama wa Wakenya, wanaoishi karibu na kambi hiyo endapo kituo hicho cha Ebola kitafunguliwa.
Serikali ya Kenya na Marekani ziliafikiana kuhusu kufunguliwa kwa kituo maalum cha kuwatibu wagonjwa wa Ebola kwa raia wa Marekani, hali ambayo imeibua hofu kuu.
Waandamanaji hao walitaka kuvunja na kuingia ndani ya kambi ya wanajeshi mjini Nanyuki.