FKF yajadili mikakati ya kuinua soka Wajir

Hussein alitoa msaada wa mipira ya soka itakayopiga jeki timu za mashinani kutoka kaunti hiyo ili kuwasaidia vijana wenye vipaji vya kandanda.

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirikisho la kandanda nchini Kenya FKF, limeanzisha mchakato wa kubuni mbinu mwafaka za kuinua viwango vya mchezo katika kaunti ya Wajir.

Haya yalibainika wakati wa mkutano baina ya Rais wa FKF Hussein Mommed na Gavana wa kaunti ya Wajir,Ahmed Abdullahi baada ya sherehe za siku kuu ya Madaraka iliyoadhimishwa katika kaunti ya Wajir.

Kinara huyo aidha, alikutana na maafisa wa soka kutoka kaunti hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti Abdinasir Mohamed Yussuf, na kujadiliana kuhusu ushirikiano baina ya afisi ya kitaifa na ule wa soka ya mashinani wa kaunti.

Hussein alitoa msaada wa mipira ya soka itakayopiga jeki timu za mashinani kutoka kaunti hiyo ili kuwasaidia vijana wenye vipaji vya kandanda.

Aidha, uwanja wa Wajir unaoselehi mashabiki 10,000, na ulioandaa sherehe za Madaraka Dei, utakuwa ukitumika kwa michezo mbalimbali ikiwemo soka .

Share This Article