Afueni baada ya wagonjwa watano kupona Ebola nchini DRC

Tom Mathinji
1 Min Read
Wagonjwa watano wapona Ebola DRC.

Wagonjwa watano waliokuwa wameambukizwa ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wametangazwa kupona na kuruhusiwa kuondoka hospitalini.

Kulingana na Taasisi ya Afya nchini humo, hatua hiyo inaleta matumaini makubwa katika kukabiliana na ugoonjwa huo ambao tayari umesababisha vifo vya zaidi ya watu 200.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo Dkt. Mwamba Kazadi, alitaja kupona kwa wagonjwa hao kuwa ushindi mkubwa unaopaswa kusherehekewa, akisema ugunduzi wa mapema na matibabu dhabiti husababisha ufanisi katika vita dhidi ya Ebola.

Mnamo siku ya Jumapili, sherehe maalum ilifanyika kwa ajili ya wauguzi wanne waliopona ugonjwa huo na kuruhusiwa kutoka hospitali.

Ugonjwa huo ulilipuka katika eneo la Ituri kaskazini mwa DRC ambapo hadi sasa zaidi ya watu 1.000 wameambukizwa, huku juhudi za kimataifa zikitekelezwa kuzima msambao wake.

Uganda imefunga mpaka wake na DRC  kama sehemu ya tahadhari, baada ya visa kadhaa kuripotiwa nchini humo.

Shirika la Afya Duniani (WHO), limesema hadi sasa hakuna dawa ya kutibu ugonjwa huo, licha ya kwamba wanasayansi wanajizatiti kupata tiba ya aina hiyo ya Ebola.

TAGGED:
Share This Article