Rais William Ruto siku ya Jumatatu amefungua vitengo vya ajali na dharura katika Hospitali ya rufaa na mafunzo ya kaunti ya Wajir.
Hospitali hiyo itakuwa ikitoa huduma mbalimbali zikiwemo matibabu ya dharura,kuwatibu na waathiriwa wa ajali kando na wagonjwa wa kawaida.
Kitengo hicho kipya kinajumuisha vitanda 12 vya sadaruki yaani ICU,vyumba vyua upasuaji,na wadi ya kisasa ya kuwalaza wagonjwa .
Hospitali hiyo inatarajiwa kuboresha huduma za afya katika kaunti hiyo ya Wajir.
Rais aliandamana na Naibu wake Kithure Kindiki na waziri wa Afya Aden Duale pamoja na viongozi wa kaunti ya Wajir.