Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini Urusi kuanzia tarehe 3 hadi 5 mwezi Juni, kufuatia mwaliko wa Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Ziara hiyo ya kihistoria ni ya pili kufanywa na Rais wa Tanzania nchini Urusi tangu Hayati Julius Nyerere, azuru taifa hilo mwaka 1969.
Rais Samia anatarajiwa kufanya mazungumzo rasmi na Rais Putin katika Ikulu ya Urusi jijini Moscow, yatakayojikita katika kuimarisha ushirikiano wa kimkakati.
Aidha, Rais Samia atashiriki na kuhutubia Jukwaa la 29 la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg (SPIEF 2026), moja ya majukwaa makubwa duniani.