Moderna kuongoza utafiti wa chanjo ya Ebola

Msimamizi wa CEPI Richard Hatchett ,alisema Jumatatu kuwa huenda chanjo ya Ebola ikawa tayari kwa majaribio ndani ya kipindi cha miezi miwili ijayo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirika la Coalition for Epidemic Preparedness Innovations (CEPI), limetangaza kutoa bajeti ya dola za Kimarekani milioni 60 sawia na shilingi bilioni 7.8 za Kenya, kwa kampuni tatu ikiwemo Moderna, MRNA.O, ili kuharakisha utafiti wa kuunda chanjo ya  virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo.

CEPI ilikuwa miongoni mwa wavumbuzi wa kwanza wa chanjo ya Covid-19.

Akizungumza na shirika la habari la Reuters, Msimamizi wa shirika hilo Richard Hatchet alisema Jumatatu kuwa huenda chanjo ya Ebola ikawa tayari kwa majaribio ndani ya kipindi cha miezi miwili ijayo.

Watu 42 wamefariki kutokana na ugonjwa wa Ebola nchini DRC kati ya wagonjwa 282 waliobainishwa huku zaidi 1,100 wakishukiwa kuwa na maambukizi kufikia sasa.

Uganda imenakili visa tisa kikiwemo kifo kimoja kutokana na ugonjwa huo ambao umetangazwa kuwa dharura na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Share This Article