Harambee Stars kuelekea Afrika Kusini leo kujipima nguvu

Harambee Stars itamenyana na Lesotho Alhamisi hii katika mchuano wa kwanza wa kirafiki katika uchanjaa wa Lucas Moripe mjini Pretoria,kabla ya kucheza mechi ya marudio Juni 7.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars, itaondoka Nairobi leo Jumannne Juni 2, kuelekea Afrika Kusini, kupiga mechi mbili za kujipima nguvu dhidi ya Lesotho.

Harambee Stars itamenyana na Lesotho Alhamisi hii katika mchuano wa kwanza wa kirafiki katika uchanjaa wa Lucas Moripe mjini Pretoria, kabla ya kucheza mechi ya marudio Juni 7.

Kocha mkuu Benni McCarthy amewajumuisha kikosini wanandinga Amos Nondi, Kelly Madada na Brian Bwire kutwaa nafasi za Job Ochieng, Ryan Ogam na Byrne Omondi waliojiondoa.

Kenya inajiandaa kwa mechi za kufuzu kwa fainali za AFCON kuanzia Septemba, wakijumuishwa kundi D, pamoja na Afrika Kusini, Guinea na Eritrea.

Mechi hizo zitakuwa za kunoa makali kwani Kenya tayari imefuzu kama waandalizi wa kipute cha AFCON cha mwaka 2027 pamoja na Tanzania na Uganda.

Share This Article