Bingwa mara mbili wa Olimpiki Eliud Kipchoge atashiriki mbio za New York City Marathon Jumapili Novemba 2, akilenga kujiunga na wanariadha walioshiriki mbio zote 6 kuu za Marathoni.
Kipchoge atalenga kujiunga na wanariadha wengine 434 walioshiriki mbio zote sita za marathoni.
Kipchoge, ambaye ameshinda mbio 11 za marathon, dhahabu mbili za Olimpiki na kukimbia chini ya saa 2 na dakika 2, anapania kukamilisha mbio za Jumapili.