Watu 21 wameripotiwa kufariki kutokana na mapropomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa katika eneo la Chesongoch, kaunti ya Elgeyo Marakwet.
Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen aliyezuru eneo hilo Jumamosi amesema kuwa watu wengine 30 hawajulikani waliko na wengine 25 wamejeruhiwa.
Shirika la Msalaba Mwekundu limesema majeruhi wengine 11 walibebwa kwa ndege ya kijeshi kupelekwa hospitalini Moi mjini Eldoret kwa matibabu.