Miamba wa soka nchini Misri, klabu ya Zamalek, wameafikiana kumtimua kocha Yannick Ferrera, kufuatia msururu wa matokeo mabovu msimu huu.
Mbelgiji huyo alipigwa teke baada ya Zamalek kusajili sare ya bao 1 na National Bank, matokeo yanayomaanisha kuwa hawana ushindi ligini msimu huu huku wakikosa kupata ushindi katika mechi nne mtawalia.
Ferrera, aliye na umri wa miaka 45,aliteuliwa Julai mwaka huu .