Serikali yawatumia msaada waathiriwa wa maporomoko ya ardhi Marakwet

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali imetuma msaada wa chakula kwa waathiriwa wa maporomoko ya ardhi katika kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Haya yanajiri huku idadi ya waliofariki kutokana na mkasa huo wa mapema Jumamosi ikifikia 21 wakati wengine 15 wakipokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Eldoret.

Akiongoza hafla hiyo, msemaji mkuu wa serikali Isaac Mwaura amesema shughuli za uokozi zinaendelea.

Maporomoko hayo ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa ya Ijumaa usiku yamekatiza usafiri katika eneo la Marakwet Mashariki.

Aidha, kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu, waliopoteza makazi kutokana na mkasa huo wamewekwa katika makao ya muda katika shule ya msingi ya Chesongoch.

Website |  + posts
Share This Article