Chui na Murang’a Seal wawika

Dismas Otuke
1 Min Read

AFC Leopards imesajili ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Mathare United katika mojawapo wa mechi za mzunguko wa nane zilizochezwa Jumapili jioni.

Vincent Mahiga and James Kinyanjui walitikisa nyavu katika dakika ya 48 na 85, huku Chui wakisajili ushindi wa tatu mtawalia ligini na kudumisha rekodi ya kutoshindwa.

Muarang’a Seal pia wakiwa nyumbani wameizidia maarifa Kenya Commercial Bank magoli 2-1.

Mabingwa watetezi Police FC wameendelea kuchechemea baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Posta Rangers huku Bidco United na APS Bomet wakitoka sare ya 1-1.

Kakamega Homeboyz pia wamebanwa nyumbani baada ya kuambulia sare ya goli 1 dhidi ya wagema mvinyo Tusker FC.

 

Website |  + posts
Share This Article