Serena Williams atarejea kucheza Tennisi ya kulipwa akiwa na umri wa miaka 44, takriban miaka minne tangu atangaze kustaafu.
Williams ambaye ni mshindi wa mataji 23 ya Grand Slam kwa mchezaji mmoja, amekubali mwaliko wa kushiriki mashindano yajayo ya Queen’s Club, yatakayoandaliwa jijini London nchini Uingereza kuanzia Jumatatu ijayo.
Hatua hiyo inaashiria uwezekano wake wa kushiriki mashindano ya Wimbledon yakatayoanza mwishoni mwa Juni.