Cherotich na Odira wawika Prefontaine Classic

Odira, aliyekuwa akishiriki Diamond League kwa mara ya pili, alitwaa ushindi wa mita 800 kwa muda wa dakika 1 sekunde 56.19.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wa Dunia Lilian Odira na Faith Cherotich walisajili ushindi katika mbio za mita 800 na mita 3,000 kuruka viunzi na maji mtawalia katika mkondo wa tisa wa mashindano ya Diamond League wa Prefontaine classic Jumamosi usiku nchini Marekani.

Odira, aliyekuwa akishiriki Diamond League kwa mara ya pili, alitwaa ushindi wa mita 800 kwa muda wa dakika 1 sekunde 56.19.

Keely Hodgkinson wa Uingereza na Mmarekani Addison Willey walimaliza katika nafasi za pili na tatu mtawalia.

Bingwa wa Olimpiki Cherotich alimpiku Winfred Yavi wa Bahrain na kuibuka kidedea katika mita 3,000 kuruka viunzi na maji kwa muda wa dakika 8 sekunde 51 nukta 71, akifuatwa na Yavi.

Bingwa mara tatu wa Olimpiki Faith Kipyegon aliambulia nafasi ya tatu katika mbio za maili moja kwa muda wa dakika 4 sekunde 17.80, akifuatwa na Dorcas Ewoi.

Share This Article