Gor Mahia yamsajili Sinisa Mihic kuwa kocha mpya

Dismas Otuke
2 Min Read

Mabingwa mara 21 wa Ligi Kuu ya Kenya, Gor Mahia FC wamemzindua Sinisa Mihic kutoka Croatia kuwa kocha mpya.

Mihic aliye na umri wa miaka 48 na anayemiliki leseni ya UEFA Pro, atasaidiwa na Zediah Otieno ambaye amekuwa kaimu kocha wa The Green Army tangu Novemba mwaka  jana  Zedekieh Otieno, pamoja na Michael Nam.

Hadi uteuzi wake, Mihic amekuwa mkufunzi wa timu za  ZK Crickvenica, inayoshiriki ligi ya daraja ya pili nchini Croatia, Al Faheel ya Kuwait, Al Shabaab FC ya Saudi Arabia, na Al Ahli Saudi FC ya Saudi Arabia.

Pia Mkroatia huyo alihudumu katika wadhfa wa Naibu kocha wa timu za Al Nasar FC ya Libya na Al Merrikh SC ya Sudan.

Hata hivyo, kocha huyo mpya anakabiliwa na mtihani mgumu wa kuwasaidia K’ogalo kuhifadhi ubingwa wa Ligi kuu ya Kenya msimu huu, wakishikilia nafasi ya tatu kwa pointi 31, baada ya mechi 18, alama 6 nyuma ya Police FC na Tusker FC wanaongoza jedwali.

Mihic ni kocha wa saba wa kigeni kuinoa Gor tangu mwaka 2020.

Roberto Oliveira Goncalves maarufu kama Robertinho kutoka Brazil aliteuliwa kocha wa Gor Mahia msimu wa mwaka 2020 na 2021 lakini akaondoka ghafla baada ya shirikisho la FKF kukataa kumuidhinisha kwani alikuwa na leseni ya CAF B.

Vaz Pinto kutoka Ureno alitwaa ukufunzi wa Gor Januari mwaka 2021 lakini pia akaojiuzulu baada ya miezi sita pekee huku Mwingereza Mark Harrison akiteuliwa Agosti mwaka 2021.

Mjerumani Andreas Spier aliteuliwa Januari mwaka 2022 lakini akaondoa mwezi Julai baada ya Gor kukataa kumwongezea mkataba na kumteua Mwingereza Jonath McKinstry aliyeisaidia K’ogalo kunyakua taji ya ligi kuu msimu wa mwaka 2023 na 2024.

Leonardo Neivas kutoka Brazil alishika mikoba ya kuwanoa Gor mwishoni mwa msimu wa mwaka 2023-2024, lakini akatimuliwa mwanzoni mwa msimu wa mwaka 2024-2025 baada ya mechi nne tu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *