Tanzania ilinakili idadi ya watalii milioni 5.36 mwaka 2024, ikizidisha lengo lake la watalii milioni tano ambalo taifa hilo lilitarajia kupata ifikiapo mwaka 2025.
Kulimngana na Waziri wa Utalii na mali asili Pindi Chana watalii milioni 3.22 walikuwa wa ndani, huku wengine milioni 2.14 wakiwa wa kimataifa.
Hata hivyo, serikali ya Tanzania ilinakili nakisi katika pato la kitaifa lililotazamiwa kutoka kwa shughuli za kitalii, ikikusanya dola bilioni 4 za Kimarekani mwaka 2024, ikilinganishwa na lengo la dola bilioni 6 kufikia Disemba mwaka huu.