Wanafunzi 8 wa Utumishi Girls Academy kufikishwa mahakamani

Tom Mathinji
1 Min Read

Wanafunzi wanane wa shule ya Utumishi Girls Academy watafikishwa katika mahakama ya Naivasha leo Jumanne kuhusiana na mkasa wa moto uliozuka Mei 28, 2026.

Moto huo ulisababisha vifo vya wanafunzi 16 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa.

Angalau wanafunzi saba wanaendelea kupokea matibabu.

Maafisa wa upelelezi wanaochunguza mkasa huo, wamefanikiwa kuwatambua wanafunzi saba wanaodaiwa kuhusika moja kwa moja katika shambulizi hilo kupitia kamera za CCTV.

Maafisa hao kutoka Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), walisema wamepiga hatua kubwa kwenye uchunguzi huo.

“Baada ya uchunguzi wa kina kupitia kamera za CCTV kwa usaidizi wa maabara katika idara ya DCI, maafisa waliweza kuwatambua wanafunzi waliowasha moto huo,” ilisema DCI.

Idara hiyo iliongeza kuwa, “Uchunguzi huo ulifanikisha kutambuliwa kwa wanafunzi saba waliohusika moja kwa moja na mkasa huo”.

Shule hiyo kwa sasa imefungwa huku Waziri wa Elimu Julius Ogamba akivunjilia mbali bodi ya usimamizi ya shule hiyo kwa kile alichokitaja kuwa kukosa kuzingatia kanuni za usalama.

Share This Article