Waziri Mkuu wa Senegal aliyetimuliwa madarakani Ousmane Sonko, ametangaza kuwa chama chake hakitakuwa ndani ya serikali mpya na kuongoza hofu ya mgawanyiko mkubwa wa kisiasa kati yake na Rais Bassirou Faye.
Kupitia mtandao wake wa X, Sonko ambaye maajuzi alichaguliwa Spika wa Bunge, alisema kuwa chama chake cha Pastef, kamwe hakitakuwa na Mawaziri serikalini.
Sonko alitoa tangazo hilo muda mfupi kabla ya mrithi wake Ahmadou Lo kutangaza baraza jipya akimdumisha Cheikh Diba wa chama cha Pastef kuwa Waziri wa Fedha.
Wadadisi wanahoji kuwa Sonko anayo mamlaka ya kuzuia ajenda kuu za serikali ya Faye kupitia kwa wadhfa wake mpya huku taifa hilo likikumbwa na mzozo mkubwa wa kifedha.