Chui wa Congo watoka nyuma na kuing’ata Uzbekistan

DRC walifuzu kwa mechi za mwondoano kwa mara ya kwanza kama mojawapo wa timu tatu bora,wakirejea katika mashindano .

Dismas Otuke
2 Min Read

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilijikatia tiketi kwa  hatua ya 32 ya Kombe la Dunia, baada ya kutoka nyuma bao moja na kuwatitiga limbukeni Uzbekistan 3-1, katika mechi ya kundi K, mapema Jumapili uwanjani Atlanta.

DRC maarufu kama Chui walijipata taabani baada ya Eldor Shomurodov ,kuwaweka Uzbekistan, kifua mbele kunako dakik ya 10 na kuongoza hadi mapumzikoni.

Awali bao la Nathanael Mbuku la dakika ya 17 lilikataliwa na mwamuzi baada ya kuotea.

Chui walirejea kipindi cha pili roho juu lakini wakawekwa pembeni hadi dakika ya 68, wakati Yoane Wissa, alipowarejesha DRC mchezoni kwa bao la kusawazisha kupitia penati.

Bao hilo liliwapa DRC ari mpya na wakaanza kwa mashambulizi kochokocho yaliyoleta faida baada ya Fiston Mayele, kupachika la pili dakika ya 78, huku Wisa akibusu nyavu kwa goli la tatu,dakika 10  kabla ya kipenga cha mwisho kupulizwa.

DRC walifuzu kwa mechi za mwondoano kwa mara ya kwanza kama mojawapo wa timu nane bora za nafasi ya tatu,wakirejea katika mashindano hayo kwa mara ya pili baada ya miaka 52.

Colombia walioongoza kundi K kwa alama 4,moja nyuma ya Ureno, baada kutoka  sare tasa katika mchuani mwingine.

Matokeo hayo yana maana kuwa DRC ni timu ya nane kati ya 10  za Afrika ,zilizofuzu kwa raundi ya 32 bora.

Share This Article