Cherotich na Wanyonyi watamba Oslo

Cherotich aliziparakasa mbio hizo kwa muda wa kasi ulimwenguni na pia rekodi mpya ya Oslo,ya dakika 9 sekunde 2.60.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mshindi wa nishani ya shaba ya Olimpiki Faith Cherotich, aliendeleza msururu wa matokeo mazuri msimu huu aliposajili ushindi wa pili wa mita 3,000 kuruka viunzi na maji mjini Oslo, Norway, Alhamisi usiku.

Cherotich aliziparakasa mbio hizo kwa muda wa kasi ulimwenguni na pia rekodi mpya ya Oslo,ya dakika 9 sekunde 2.60.

Winfred Yavi wa Bahrain, alimaliza wa pili kwa dakika 9 sekunde 2.76, huku Marwa Bouyazani wa Tunisia akiridhia nafasi ya tatu.

Bingwa wa Olimpiki Emmanuel Wanyonyi, alisajili ushindi wa kwanza wa Diamond League msimu huu, aliposhinda mita 800 kwa dakika 1 sekunde 42.78,akifuatwa na Mohammed  Attaoui wa Uhispania, kwa dakika 1 sekunde 42.90, huku Djamel Sedjati kutoka  Algeria akiambulia nafasi ya tatu.

Mkenya Timothy Cheruiyot alimaliza wa nne katika mbio za maili moja zilizoshindwa na Mreno Isaac Nader.

 

Website |  + posts
Share This Article