Timu ya taifa ya Kenya ya soka ya wanawake Harambee Starslets ,ilijipiga kifua licha ya kushindwa kwenye fainali ya mashindano ya FIFA Series na Australia 2-0, jana jioni katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.
Starlets walidhidhirisha mchezo wa hali ya juu kutoka mwanzo hadi mwisho huku wakiwabana Matildas ya Australia kwa kipindi kirefu.
Kiungo wa Starlets Mwanahalima Adam alisema licha ya kushindwa mechi hiyo iliwapa matumaini ya kufuzu kwa kombe la Dunia siku moja.
India iliwazabua Malawi 3-2 na kumaliza katika nafasi ya tatu.