Viongozi wa upinzani nchini Kenya walikuja kwa matao ya juu siku ya Jumatano wakiitaka serikali kufutilia mbali mpango wake wa ununuzi mafuta wa G to G, ukisema umechangia kuongezwa kiholela kwa bei ya mafuta nchini.
Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka,kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua,kiongozi wa DP Justin Muturi,Kiongozi wa DAP-K,Eugine Wamalwa na kiongozi wa Jubilee Fred Matiangi kwa kauli moja waliikashifu serikali kwa kuchangia kupanda kwa bei ya bidhaa za mafuta.
Waliapa kuitisha maandamano ya kitaifa kuishiniza serikali endapo haitafutilia mbali mpango wa sasa wa kununua mafuta.
Aidha,walitaka kujiuzulu mara moja wa Waziri wa kawi Opiyo Wandayi, na wote wanaodaiwa kuhusika kwenye Sakata ya mafuta ya wiki iliyopita.