Oburu kutetea kiti chake cha Useneta Siaya 2027

Martin Mwanje
1 Min Read
Seneta wa Siaya Dkt. Oburu Oginga

Seneta wa kaunti ya Siaya Dkt. Oburu Oginga atatetea wadhifa huo kwa tiketi ya chama cha ODM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. 

Dkt. Oburu, mwenye umri wa miaka 82, ametangaza hayo leo Jumatatu jijini Kisumu alipokutana na wanaopania kugombea viti mbalimbali kwenye uchaguzi huo.

Mrengo wake wa ODM umeashiria kuwa chama hicho kitamuunga mkono Rais William Ruto kugombea muhula wa pili kwenye uchaguzi ujao.

Wakati wa mkutano huo, Gavana wa Homa Bay Gladys Wanga pia ameashiria atatetea wadhifa wake kwa tiketi ya ODM.

Wanga huenda akakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Naibu wake wa zamani Joseph Oyugi Magwanga waliyetalikiana kisiasa miezi michache iliyopita.

ODM imeahidi zoezi huru la mchujo wa wagombea wa chama hicho na kutaka ngome zake kutoshindaniwa na UDA, chama mshirika katika serikali jumuishi.

Kwa upande wake, UDA imeashiria kuwa itawasilisha wagombea katika kila pembe ya nchi.

Share This Article