Spika wa bunge la Senegal El Malick Ndiaye amejiuzulu, siku mbili tu baada ya rais wa taifa hilo kumfuta kazi Waziri Mkuu, Ousmane Sonko.
Ndiaye alisema hapo jana kuwa kuondoka katika wadhfa wake, ni uamuzi wake binafsi na amezingatia maslahi ya taifa.
Spika huyo ni miongoni mwa wanachama wa chama cha PASTEF kinachoongozwa na Sonko, na kina wawakilishi wengi bungeni.
Kuondoka kwa Ndiaye, kunazidisha msukosuko wa kisiasa ambao tayari unatokokota katika taifa hilo la Afrika Magharibi.
Kulingana na wachambuzi, huenda Rais wa Senegal Diomaye Faye, akapata wakati mgumu kuingoza taifa hilo na kupitisha sheria kutokana na wengi wa wawikilishi wa bunge kuwa wanachama wa PASTEF.
Rais Faye alimfuta kazi Waziri mkuu Ousmane Sonko siku ya Ijumaaa, baada ya miezi kadhaa ya mvutano baina ya viongozi hao wawili.
Taarifa ya BBC