Ratiba ya 16 bora Kombe la Dunia yakamilika, Morocco wakifungua na Canada leo

Morocco watafungua hatua hiyo Jumamosi usiku dhidi ya Canada mjini Houston, Marekani kuanzia saa mbili usiku.

Dismas Otuke
1 Min Read

Ratiba ya mechi za raundi ya 16 bora imebainika kufuatia kukamilika kwa mechi za raundi ya 16 bora mapema Jumamosi.

Morocco watafungua hatua hiyo Jumamosi usiku dhidi ya Canada mjini Houston, Marekani kuanzia saa mbili usiku kabla ya Ufaransa kukabiliana na Paraguay saa sita usiku wa manane katika uwanja wa Philadephia.

Jumapili itakuwa zamu ya Brazil kukabiliana na Norway  saa tano usiku katika uwanja wa New Jersey, huku wenyeji Mexico wakiwa nyumbani dhidi ya Uingereza Jumatatu saa tisa alfajiri.

Majrirani na waandalizi wenza wa makala yajayo Ureno na Uhispania, watakutana katika mechi ya Jumatatu usiku mjini Dallas.

Wenyeji Marekani watacheza na Ubelgiji Jumanne Julai 7, saa tisa alfajiri katika uga wa Seattle, kabla ya Argentina kukabana koo na Misri katika uchanjaa wa Atlanta Julai 7, kuanzia saa moja usiku.

Uswizi na Colombia watakamilisha raundi hiyo Jumanne, Julai 7 kaunzia saa tano usiku uwanjani Vancouver, Canada.

Share This Article