Police FC kukabiliana na Tusker FC fainali ya kombe la Mozzart bet

Fainali ya kombe hilo itapigwa Juni 14, huku mshindi akiwahi tiketi ya kuiwakilisha Kenya katika mashindano ya Kombe la Shirikisho msimu ujao.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wanaoondoka wa Ligi kuu Kenya,Police FC watamenyana na Tusker FC, kwenye fainali ya Kombe la Mozzart Bet, baada ya kushinda nusu fainali Jumamosi.

Tusker FC walihitaji matuta ya penati ili kuwashinda Kenya Commercial Bank, mabao 4-3, baada ya sare tasa.

Police FC wamejikatia tiketi kwa fainali pia baada ya kuwalemea Bandari FC, magoli 5-3, kupitia penati baada ya sare kappa.

Fainali ya kombe hilo itapigwa Juni 14, huku mshindi akiwahi tiketi ya kuiwakilisha Kenya katika mashindano ya Kombe la Shirikisho msimu ujao.

Share This Article