Mfanyabiashara Bilionea wa Nigeria Aliko Dangote, aliwasili jijini Dar es Salaam,kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu kiwanda cha mafuta anachodhamiria kufungua mkoani tanga.
Kiwanda hicho kinatarajiwa kugharaimu dola za Kimarekani kati ya bilioni 15 na 17 na kitalkuwa na uwezo wa kuchakata mapipa 650,000 ya mafuta kwa siku punde kitakapokamilika.
Ziara ya Dangote inafuatia kikako cha hivi maajuzi baina ya Rais william Ruto, wa Kenya, na Samia katika Ikulu ya Dar es Salaam, baada ya kongamano la African we build lilifonyika Nairobi mwezi jana .
Kenya na Tanzania, zinaendeleza juhudi za kumshawishi bwenyenye huyo kufungua kiwanda hicho ambacho kitafungua fursa nyingi kwa mataifa hayo ya Afrika mashariki, na kuchangia kupunguza gharama ya uagizaji mafuta kutoka nje ya nchi na Kenya na Tanzania.