Moshi mweusi umefuka tena leo kutoka dohani la Sistine mjini Vatican-makao makuu ya kanisa Katoliki, kuashiria kuwa makadinali 133, wanaopiga kura hawajaafikiana kuhusu uteuzi wa Papa Mtakatifu mpya.
Jana pia moshi mweusi ulionekana ishara kuwa kumekuwa na vuta ni kuvute katika mchakato huo wa upigaji kura.
Mshindi ni sharti apate kura 88 kati ya kura 133 zinazopigwa na makadinali kutoka mataifa 90 ulimwenguni.
Makadinali hao wana hadi kesho Ijumaa kumchagua Papa Mtakatifu mpya kumrithi marehemu Papa Francis.