Korti kuamua kesi ya kuondolewa kwa kituo cha kitaifa cha ujumuishaji kura

Seneta wa Busia Okiya Omtatah anataka mahakama kufutilia mbali kituo hicho kwa madai kuwa matokeo ya urais yanayotangazwa katika eneo bunge ni ya mwisho kulingana na katiba ya mwaka 2010.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mahakama Kuu inatarajiwa kutoa uamuzi wa kesi iliyowasilishwa na Seneta wa Busia Okiya Omtatah ya kupinga kuwepo kwa kituo cha kitaifa cha kujumuisha matokeo ya kura za urais.

Kwenye kesi hiyo, Omtatah anashikilia kuwa matokeo ya urais yanayotangazwa katika eneo bunge ni ya mwisho kulingana na katiba ya mwaka 2010.

Omtatah anataka mahakama iharamishe na kufutilia mbali kituo cha kitaifa cha kujumuisha matokeo ya kura za urais.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka  (IEBC) imekuwa ikiendesha kituo cha kitaifa cha ujumuishaji kura za urais katika ukumbi wa Bomas of Kenya kila mwaka wa uchaguzi mkuu.

Share This Article