Benki Kuu ya Kenya(CBK) iliadhimisha miaka 60 tangu kubuniwa kwake Alhamisi usiku,katika hafla iliyohudhuriwa na William Ruto.
Hafla hiyo iliamndaliwa katika chuo cha kutoa mafunzo ya usimamizi wa fedha nchini katika barabara kuu ya Thika.
Rais Ruto alisifia jukumu muhimu la CBK kuhakikisha uthibati wa kifedha nchini ikiwemo wakati wa kupanda kwa bei ya kubadilisha Dola ya Marekani.
Aliongeza kuwa CBK imethibiti bei hiyo ambapo kwa sasa Dola moja inanuliwa kwa shilingi 129,huku mfumko wa bei za bidhaa ukisalia asilimia 6.6 katika mwezi wa Agosti.
Rais aliataja pia CBK imezisaidia benki za kibiashara kutoa mikopo kwa wateja wake ambayo imechangia kuimarika kwa maisha ya familia,kuongeza uwekezaji,kubuni nafasi za ajira na kukuza uchumi wa nchi.