KPLC yanakili faida ya asimilia 2.5 kufikia Juni mwaka huu

Aidha,hisa za KPLC ziliimarika kutoka shilingi 12.81 mwaka huu kutoka kwa shilingi 12.54 mwaka uliotangulia kwa kila hisa.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kampuni ya usambazaji umeme nchini Kenya Power(KPLC) ilinakili faida ya asilimia 2.5, ikiwa sawa na shilingi bilioni 25 katika mwaka wa kifedha uliokamika Juni 30 mwaka huu.

Faida hiyo ilipanda kutoka shilingi bilioni 24.5, ambazo KPLC ilirekodi katika mwaka uliotangulia wa 2024/2025.

Aidha,hisa za KPLC ziliimarika kutoka shilingi 12.81 mwaka huu kutoka kwa shilingi 12.54 mwaka uliotangulia kwa kila hisa.

Kutokana na ufanisi huo KPLC imetangaza kuongeza marupurupu ya hisa zake kwa asilimia 50.

Pia deni las kampuni hiyo lilishuka kutoka shilingi bilioni 87.6 mwaka uliotangulia hadi shilingi bilioni 79.8, katika mwaka wa kifedha uliokamika Juni 30 mwaka huu.

TAGGED:
Share This Article