Bei ya petroli na dizeli yashuka kwa takriban shilingi 5 nchini Tanzania

Hata hivyo, serikali imewaonya wenye mafuta kutoongeza bei wala kuuza bidhaa hiyo kwa bei za chini kuliko zilizowekwa na EWURA.

Dismas Otuke
1 Min Read
EPRA yapunguza bei ya diesel, bei ya Petroli na Mafuta Taa zakosa kubadilika.

Serikali ya Tanzania imetangaza bei mpya za mafuta ya petroli na dizeli zitakazotumika mwezi huu wa Septemba.

Kulingana  na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) bei mpya ya petroli imeshuka kwa shilingi 4.98, sawa na shilingi 102 za Tanzania  huku ile ya dizeli ikiuzwa kwa 4.93, sawa na shilingi 101 kwa kila lita moja.

EWURA imetangaza kuwa lita moja ya petroli jijini Dar es Salaam itakuwa shilingi 3,796 za Tanzania sawa na shilingi 185.39, huku dizeli ikiuzwa kwa shilingi 3,877 za Tanzania sawa na shilingi 189.34 za Kenya.

Hata hivyo, serikali imewaonya wenye mafuta kutoongeza bei wala kuuza bidhaa hiyo kwa bei za chini kuliko zilizowekwa na EWURA.

Bei hizo zinatarajwia kuzuia kupanda kwa gharama za usafiri kwa kutumia magari ya umma.

TAGGED:
Share This Article