Tusker FC wameondoka nchini Jumatano jioni keulekea Kigali,Rwanda, kwa mkumbo wa kwanza wa mchujo wa kwanza kuwania kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahli Madani .
Tusker watakabiliana na Al Ahli Madani Jumamosi hii Septemba 5, huku marudio yakipigwa Septemba 12 jijini Nairobi.
Wagema Mvinyo Tusker wanarejea kwenye kipute hicho kwa mara ya kwanza baada y kuwa nje kwa miaka minne ,mara ya mwisho wakishiriki ikiwa msimu wa mwaka 2021/2022.
Aidha,Tusker wanajivunia kucheza hadi fainali ya Kombe hilo mwaka 1994.
Tusker walifuzu kuiwakilisha Kenya baada ya kunyakua Kombe la Mozzart Bet.